Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa ushauri wake kwa kiongozi mkuu wa nchi ili kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo.
Zitto
ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook, japo hakutaja jina lakini
maelezo yake yanaonesha kuwa mwenye uwezo wa kufanya maamuzi hayo ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, ndiye mlengwa wa ujumbe
huo.
Hivi ndivyo alivyoandika:
“Thomas Sankara once said
“You cannot carry out fundamental change without a certain amount of
madness”. Uwendawazimu
1) Weka mikataba yote ya Rasilimali za Nchi wazi –
PSAs and MDAs 2) Futa posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali
kama Mpango wa Maendeleo unavyotaka
3) Futa business
class air tickets Kwa watendaji wa Serikali na wanasiasa isipokuwa Rais,
Makamu wa Rais, Waziri Mkuu
4)Futa matumizi ya mashangingi ( BoT
wameonyesha mfano kwenye hili )
5 )Futa uagizaji wa sukari kutoka Nje na
anzisha miradi ya miwa tuuze sukari Nje
6 )Weka wazi taarifa ya Serikali
kuhusu utoroshaji wa fedha na fungua mashtaka Kwa wahusika mara moja
7
)Wape takukuru mamlaka ya kukamata na kushtaki na kila mwenye Mali
athibitishe yeye kaipataje (reverse burden of proof )
8 )Mali na Madeni
ya Viongozi yawe wazi Kwa umma na wananchi waruhusiwe kuhoji
9 )Ruhusu
mshindi wa uchaguzi Zanzibar atangazwe na ufanye naye kazi
10)Acha
mchakato wa Katiba Kwa kuanzia alipoishia Warioba, achana na Katiba
Pendekezwa.”
"Thomas Sankara once said “You cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness”. Uwendawazimu 1)...
Posted by Zitto Kabwe on Tuesday, November 10, 2015
Post a Comment