Siku chache baada ya kufuta safari za vigogo nje ya nchi,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli anakusudia kufyeka wizara 8 miongoni mwa 28 zilizopo sasa ili kubana matumizi.
Hatua
hiyo ya Dr Magufuli ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi
alizozitoa kwa wananchi wakati akijinadi kwenye kampeni zake za
kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi-CCM kwamba atapunguza
ukubwa wa serikali kwa kuunda baraza dogo la mawaziri.
Katika
miaka 10 ya uongozi wa Rais Kikwete, kumekuwa na malalamiko ya
ukubwa wa baraza la Mawaziri huku baadhi ya wizara zikiwa na
mawaziri watatu.
Kwa
mkakati huo,endapo Dr Magufuli ataweza kufyeka Wizara 8, maana
yake atakuwa amewatupa nje ya ajira vigogo zaidi ya 20 ambao
ni mawaziri na manaibu wao pamoja na makatibu wakuu na
manaibu wao ambao kasma zao za mishahara ni mzigo mkubwa kwa
serikali
Baraza
la kwanza la Rais mstaafu Kikwete mwaka 2005 lilikuwa na
Mawaziri na Manaibu wao 60, jambo ambalo lililalamikiwa na wadau
wengi kwamba halina tija bali lilikuwa na lengo la kulipana
fadhila
Taarifa
zaidi zinasema kuwa huenda Rais Magufuli akachelewa uteuzi wa
mawaziri hadi Disemba mwaka huu ili kujipa muda zaidi wa
kuangalia na kufanya uchambuzi wa wizara zipi za kuzifyeka
kwani baadhi hazina tija
Wizara zilizo Hatarini Kufyekwa
Ingawa
Rais Magufuli hajazitaja Wizara zitakazofyekwa, lakini habari
toka serikalini zinasema kuna uwezekano mkubwa wizara zisizo na
tija na zinazoweza kuunganishwa na kuwa idara chini ya wizara
fulani, zikafyekwa.
Wizara
hizo ni Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto ambayo huenda
ikaingizwa kwenye ofisi ya Makamu wa Rais, hasa wakati huu
ambapo ofisi hiyo inashikiliwa na mwanamke.
Nyingine
ni wizara iliyokuwa ikishughulika na mambo ya utawala bora
ambayo wadadisi wa masuala ya siasa wanapendekeza iwe chini ya
Wizara ya mambo ya ndani pamoja na Takukuru ili kukabiliana
na Rushwa.
Wizara
ya Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira nayo inaweza
kufyekwa na suala la Mazingira likasimamiwa na kila Wizara kwa
kuwa na kitengo chake cha kusimamia mazingira badala ya kuwa
na Waziri wake.
Wizara
ya uwekezaji na uwezeshaji huenda ikafutwa na kuingizwa ndani
ya kituo cha uwekezaji ( TIC ) na kuwa idara nyeti ya
kusimamia maswala ya uwekezaji ikiwa chini ya wizara ya
Viwanda na Biashara.
Wizara
ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo nayo inapumulia mashine
kwani huenda ikaungana na Idara ya Habari (Maelezo) na kuwa
idara zilizo chini ya ofisi ya Waziri mkuu badala ya kuwa
Wizara kamili
Wizara
ya Kilimo na Mifugo inapendekezwa kuwa moja badala ya mbili
kama ilivyosasa.Waziri katika ofisi ya Rais (Kazi Maalumu)
iliyokuwa inashikiliwa na Profesa Mwandosya yenyewe imekufa kifo
cha Mende,kwani hakuna ubishi kwamba itafyekwa.
Post a Comment