Cristiano Ronaldo kuingia katika headlines imekuwa kawaida sana kwake ukilinganisha na Lionel Messi ambaye amekuwa akitajwa kama mshindani wake mkubwa licha ya kuwa maisha binafsi wako tofauti sana kitabia za nje ya uwanja. Ronaldo amekuwa akihusishwa sana kuwa katika mahusiano na wapenzi wengi kwa nyakati tofauti tofauti.
Amewahi kuripotiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi ya muda mfupi na Kim Kardashian lakini Paris Hilton amewahi kutoka na staa huyo, mrembo kutoka katika mchezo wa tennis Maria Sharapova na baadae Iryna Shayk ila headlines za November 17 zinazo muhusu staa huyo anatajwa kutoka kimapenzi na Marisa Mendes ambaye ni binti wa wakala wake Jorges Mendes.
Ronaldo ambaye alikuwa akitajwa kuwa single toka aachane na mpenzi wake mwanatindo wa Urusi Iryna Shayk, vyombo vingi vya habari vya Ureno vimekuwa vikimtaja kutoka na mtoto wa wakala wake Jorges Mendes. licha ya Ronaldo kutokiri kuwa na mpenzi mpya katika interview yake alioifanya hivi karibuni baada ya kuulizwa kuhusu mahusiano.
“Kuwa na mpenzi sio kazi rahisi kiukweli najua asilimia hamsini wanakupenda kwa sababu ya umaarufu ni kawaida na hiyo sio kwangu peke yangua hata watu maarufu wengine hutokewa na tatizo hilo” >>> Ronaldo
Post a Comment