January 15 2016 ndio inaelekea mwisho wa
siku lakini habari ni wakati wowote, inaponifikia mpya yoyote ni jukumu
langu pia kuhakikisha haupitwi na hauchelewi pia kujua kinachoendelea
Ninayo ripoti ya Mwanza, kumekuwa na vichwa vya habari kuhusu watendaji kadhaa kusimamishwa kutokana na sababu mbalimbali, maamuzi ya Rais Magufuli yameigusa Mwanza leo…
Rais Magufuli amemsimamisha kazi Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Faisal Issa kwa
tuhuma za ukosefu wa nidhamu aliouonesha wakati wa kikao cha Kamati ya
Usalama ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alikuwa mmoja ya waliokuwemo
kwenye kikao hicho.
Post a Comment