Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amewataka
viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoingilia
mgogoro uliopo ndani ya chama hicho kwa sababu hauwahusu.
Kauli
hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na
wanachama wa chama hicho katika kikao cha ndani, kilichofanyika Wilaya
ya Kinondoni ambapo alisema Chadema kushindwa kutekeleza Operesheni
Ukuta ni dhahiri chama hicho kimeshindwa kutekeleza kile wanachoahidi
kwa Watanzania.
Alisema
mpaka sasa kumekua na vikao mbalimbali vinavyofanywa na viongozi wa
Chadema kwa ajili ya kuivuruga CUF, jambo ambalo alisema haliwekezani.
“Chadema
wanajitahidi kutuvuruga kwa kutuma waasi wa chama hiki, lakini naomba
niwaambie hawawezi, CUF ni ngangari hata serikali inajua na
wanachokifanya ni kupoteza muda bure.
“Unajenga Ukuta wa biskuti, ukiumwagia juisi unamong’onyoka, Ukuta gani huo, huu muziki wa CUF ni ngangari hawauwezi,” alisema Lipumba.
Alisema
katika kipindi hiki ambacho wana kesi mahakamani, wanachama wa chama
hicho wataendelea na shughuli za kukijenga chama hicho pamoja na
kuwasisitiza kuwa na msimamo wa kutetea chama na katiba yake, jambo
ambalo linaweza kuwasaidia kufikia malengo waliyokusudia ya kushika dola
kafika Uchaguzi wa mwaka 2020.
Alisema
kutokana na hali hiyo, rasilimali za chama hicho zinasimamiwa kwa
umakini chini ya walinzi wa chama hicho, Blue Guard ambao Katibu Mkuu wa
chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alisema ni wavamizi hawatambui.
“Ninamshangaa
Maalim Seif sasa hivi anaibuka na kusema hawatambui walinzi wa chama
Blue Guard ambao miaka yote walikua wanamlinda pamoja na rasilimali za
chama, lakini hayo yamekwisha nitazidi kumwomba aje tujenge chama hata
kama kesi inaendelea mahakamani,” alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano anayemunga mkono
Profesa Lipumba, Abdallah Kambaya alisema kupoteza nafasi ya umeya na
naibu wake katika Manispaa ya Kinondoni ni matokeo ya mgogoro wa CUF na
kutokuwepo ushirikiano ndani ya Ukawa.
“Maalim
Seif anaunga mkono Ukawa, mbona wanachama wa Ukawa wameshindwa
kutusaidia ili kupata meya na naibu wake kwenye uchaguzi wa leo?
(jana),” alihoji.

Ukiwa umefanya kazi maisha yako yote kujenga familia na urithi, huwezi kuruhusu kivuli cha mtu wa tatu kiiharibu katika miezi michache tu. Niligundua kuwa mabadiliko ya ghafla ya tabia ya mume wangu yalikuwa kuingiliwa kiroho, si tu mgogoro wa katikati ya maisha.
ReplyDeleteNiliwasiliana na Mystic Kakaa kwa ajili ya uingiliaji kati wa kibinafsi. Kazi yake ilikuwa ya upasuaji. Alitambua kivuli na kukiondoa kabisa bila drama yoyote ya umma. Ndani ya siku 5, umakini wa mume wangu ulirudi nyumbani kwetu na katika mustakabali wetu. Ikiwa unalinda maisha yenye thamani kubwa na unahitaji bwana anayeelewa busara, wasiliana naye kwa: dawnacuna314@gmail.com
WhatsApp: +2349046229159
Yeye ndiye kiwango cha dhahabu.
Kwa uchawi wa upatanisho wa uhusiano/ndoa.
Uchawi wa kumfanya mpenzi wako wa zamani/mwenzi wako aombe msamaha.
Uchawi wa kumrudisha mpenzi wako/kumvutia mpenzi mpya.
Uchawi wa kurejesha mali/pesa zilizoibiwa.
Mabadiliko ya umbo/Uchawi wa kutoweka.
Uchawi wa kushinda bahati nasibu/kesi ya mahakama. Na zaidi